Jumatano , 17th Dec , 2014

SHIRIKISHO la Soka nchini TFF limesema programu ya Grassroots inayoendeshwa kwa vitendo itawasaidia walimu wanaoshiriki kozi hiyo kuitumia katika shule mbalimbali hapa nchini na kuweza kupata wanafunzi wenye vipaji vitakavyoweza kukua.

Akizungumza na East Africa Radio,Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF,Salum Madadi amesema katika Programu hiyo wamechukua wanafunzi zaidi ya 200 kutoka shule ya Msimbazi yeye Programu hiyo ambao wanapewa mafunzo na washiriki wa kosi hiyo ambao ni walimu kutoka shule za Msingi Mkoani morogoro,Pwani na Dar es salaam.

Madadi amesema mafunzo hayo pia yatawasaidia wanafunzi hao kuendelea kuwa na uelewa kuhusuana na michezo hususani soka hivyo kuweza kuwa na uelewa mkubwa pindi watakapomaliza shule na kupata ajira kirahisi.