Muonekano wa jezi za sasa za Taifa Stars
Taarifa kutoka Shirikisho hilo inasema kuwa TFF imefungua milango kwa umma ambako mtu mmoja mmoja anaweza kuwasilisha ubunifu wa muonekano wa jezi hizo katika ofisi zake zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imesema kuwa mwisho wa kupokea zabuni hizo ni Novemba 30, 2016, na kuweka sharti kwa mbunifu kutoiga ubunifu kutoka makampuni makubwa ya vifaa vya michezo.
Imesema mbunifu bora au mshindi wa jezi ambazo zitakuwa lazima ziwe na nembo ya TFF na Bendera ya Taifa, atazawadiwa shilingi milioni mbili (Sh milioni 2).
Jezi za sasa za Timu ya Taifa ni rangi ya bluu kwa michezo nyumbani na nyeupe mechi za ugenini.