TFF yashtukia hujuma mechi ya Yanga Vs Ngaya

Friday , 17th Feb , 2017

Kuelekea katika mchezo wa marudiano mzunguko wa awali Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Ngaya hapo kesho Jumamosi, Shirikisho la Soka nchini TFF limetoa onyo kwa mashabiki waliopanga kubeba mabango yenye ujumbe wa kuikashifu serikali.

Mashabiki Yanga

 

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema, wamepokea taarifa kwamba wapo mashabiki ambao wamepanga kubeba mabango yenye ujumbe tofauti wa kuikashifu serikali pamoja na TFF suala ambalo litachangia vurugu katika mchezo huo hapo kesho.

Alfred amesema, iwapo wahusika watakaofanya matukio yoyote ya kupoteza amani uwanjani hapo kesho pamoja na katika mchezo wa Februari 25 katika mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga hatua kali za kisheria zitachukuliwa watuhumiwa kufikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka ya kosa la jinai.

Wakati huohuo Alfred amesema kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania Serengeti Boys kitavunja kambi kwa muda wa wiki mbili kuanzia Februari 25 mpaka Machi 12 mwaka huu ili kutoa mapumziko mafupi kwa vijana hao kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya kuelekea kwenye mashindano ya AFCON ya vijana nchini Gabon.

Huyu hapa Alfred akielezea...