Jumatano , 29th Sep , 2021

Nyota wa zamani wa NBA, Hasheem Thabeet ameendelea kuwa gumzo baada ya usiku wa jana kuisaidia timu yake ya Savio kuibuka na ushindi wa alama 83-69 dhidi ya ABC kwenye game 3 ya RBA kwa kufikisha alama 32, rebound 22, assist 6 na kuzuia mipira mara 2.

[Hasheem Thabeet akiwa na timu yake ya Hsinchu JKO Lioneers kwenye ligiya kikapu nchini Taiwan msimu ulioisha wa mwaka 2020-2021.]

Ushindi huo unaiFanya Savio kuongoza series ya fainali RBA kwa 2-1 baada ya kupata ushindi wa alama 82-73 dhidi ya Army Basketball Club ‘ABC’ kwenye game 1 kabla ya ACB kupata ushindi wa alama 84-79 na kufanya series kuwa 1-1 kwenye game 2 Jumatatu yawiki hii.

Wawili gao wanataraji kushuka dimbani tena 2:00 usiku wa leo Septemba 29, 2021 kwenye uwanja wa Don Bosco Oysterbay ulioppo Jijini Dar es Salaam huku wengi wakianza kumtazama Thabeet kama MVP wa fainali hizo.

Kwa upande wa RBA ya  Wanawake, timu ya Vijana Queens wamefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwa kuifunga JKT Stars alama 68-63 na kufanya series kuwa 2-1 na kuwapunguza kasi Vijana Queens. Game 4 ya RBA ya wanawake itapigwa saa 12:00 jioni ya leo kwenye uwanja wa DB Oysterbay.