Jumamosi , 10th Mei , 2025

Mabingwa wa ligi kuu ya wanawake England Chelsea wamekuwa timu ya kwanza ya wanawake kumaliza msimu bila kufungwa baada ya hii leo kushinda 1-0  dhidi ya Liverpool na kukabidhiwa kombe mbele ya mashabiki wao kwenye dimba la Stamford Bridge .

Timu ya wanawake ya Chelsea

Muingereza Aggie Beever-Jones alifunga bao la ushindi dakika za lala salama, akipiga mpira uliompita kipa Rachael Laws na kuumaliza msimu wa 2024-2025 kwa historia.

The Blues wameshinda michezo 19 na kutoka sare tatu katika mechi 22 katika msimu wa kwanza wa kocha wao  Mfaransa Sonia Bompastor's  .

Chelsea walitangaza ubingwa wao wa WSL  Aprili 30 wakiwa wamesalia na michezo miwili na bado wanawinda Treble katika fainali ya kombe la FA itakayofika Mei 18