Ijumaa , 13th Dec , 2019

Timu ya Baobab Queens ya mkoani Pwani ambayo inashiriki ligi kuu ya soka ya wanawake Tanzania, imekwama katika Kijiji Cha mabeshi KM115 kabla ya kufika Tabora ikiwa inaelekea Kigoma.

Gari na baadhi ya wachezaji wa Baobab Queens

Safari hiyo imekwama baada ya gari walilokuwa wakisafiria kushika moto kutokana na hitilafu za mfumo wa umeme kwenye gari. 

Timu hiyo inaelekea mkoani Kigoma kwenye mchezo wa ligi kuu ya wanawake dhidi ya Kigoma Sisters utakaopigwa kesho.

Mpaka mchana huu wa Desemba 13, 2019, wachezaji wa timu hiyo na benchi la ufundi bado wapo Mabeshi ambapo mafundi wanaendelea kufanya marekebisho ili waweze kuendelea na safari.