Timu ya taif aya Kriketi, Tanzania.
Timu hiyo inayoongozwa na Kocha Steve Tikolo ambaye ni raia wa Kenya, atakiongoza kikosi hicho chenye orodha ya wachezaji kumi na sita (16), kutoka kwenye ligi kuu ya Tanzania maarafu kama Caravan T20, iliyotamatika hivi karibuni.
Akizungumzia faida ya michuano hiyo, ambayo Tanzania wamealikwa na wenyeji Kenya, Tikolo ametabanaisha kuwa itakuwa fursa kwake kuona maendeleo ya wachezaji na kuongeza ubora kwenye sehemu ambazo zinamapungufu.
Kocha huyo mwenye uzoefu wa mchezo wa Kriketi nchini, amesema kuwa amefurahishwa na timu yake kwenye upande wa maendeleo ya kiwanjani, akielezea kulidhishwa na Mikimbio, Urushaji wa mipira pamoja na upigaji wa mipira inayorushwa.
Baada ya mashindano hayo nchini Kenya, Timu ya Tanzania itaelekea nchini Rwanda kwenye michuano itakayowakutanisha mataifa ya Afrika ambapo watawania nafasi mbili za kushiriki kombe la dunia nchini Australia 2022.
Kwa Upande wa Nahodha wa timu ya Taifa, Abhik Patwa amesema kuwa ari na morali ya wachezaji ipo juu sana ambapo wameonesha utayari na kuelekea kwenye mashindano ya majaribio nchini Kenya, na baadaye kwenye kusaka tiketi za kucheza fainali za kombe la dunia nchini Rwanda.






