Jumatatu , 5th Mar , 2018

Baada ya maamuzi ya mchezo wa ligi kuu jana kati ya Lupuli FC dhidi ya Ndanda FC kugubikwa na utata, Kocha wa Ndanda FC Malale Hamsini, amesema timu yake haijafungwa na Lipuli bali imefungwa na Mwamuzi.

Hamsini amesema hayo baada ya timu yake ya Ndanda FC kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Lipuli FC hivyo kupoteza alama tatu muhimu ambapo amesisitiza kuwa amekubali matokeo na anaheshimu maamuzi ya refarii.

''Hatujafungwa kihalali kwenye mchezo, watu wote waliojaa uwanjani wamejionea kuwa mwamuzi ametuonea na sisi hatujafungwa na Lipuli tumefungwa na mwamuzi'', amesema.

Baada ya matokeo hayo ya jana Lipuli FC imerudi kwenye nafasi ya 7 ikiwa na alama 23 kwenye michezo 20 huku Ndanda FC ikiwa na alama 18 baada ya mechi 20. Majimaji inaburuza mkia ikiwa na alama 15.