
Rais wa Klabu ya Barcelona , Josep Maria Bartomeu akimkabidhi jezi aliyekua mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Eric Abidal.
Taarifa hiyo inakuja siku moja baada ya Klabu hiyo kutangaza kumtimua kazi kocha Quiquie Setien ambaye ndiye aliyekiongoza kikosi hicho katika mchezo wa robo fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya waliopoteza kwa fedheha kwa kipigo cha aina yake cha bao 8 kwa 2 dhidi ya Bayern Munich.
Barceloa inatajwa ipo katika mpango wa kufanya mabadiliko katika idara ya ufundi ili kuijenga Timu hiyo itakayoleta ushindani msimu ujao.