Ijumaa , 14th Aug , 2020

Mlinzi wa kulia wa Liverpool Trent Alexander Arnold ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana wa ligi kuu England EPL msimu uliomalizaika wa 2019-20.

Trent Alexander-Arnold mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana wa ligi kuu England EPL, akipiga mpira wa adhabu kwenye moja ya michezo akiwa na Liverpool.

Tuzo ya mchezaji bora kijana wa ligi kuu England EPL hutolewa kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 23 au chini ya umri huo, Mshindi hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.

 

Katika tuzo hii walikuwa wanawania wachezaji nane na Ttrent akapigiwa kura nyingi na kuibuka mshindi. Wachezaji wengine ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo ni Anthony Martial, Marcus Rashford na Mason Greenwood wote wa Manchester United, Jack Grealish wa Aston Villa, Christian Pulisic na Mason Mount kutoka Chelsea na goli kipa Dean Henderson wa Sheffield United.

 

Trent alikuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi cha liverpool msimu huu wakichukua ubingwa wa ligi kuu ya England EPL kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 30. Mlinzi huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 21 alicheza michezo yote 38 ya ligi akifunga mabao manne na kutoa pasi za usaidi wa mabao yani Assists 13.