Cannavaro amesema hayo baada ya timu yake kuchapwa na Mbao walipokutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya Nusu Fainali kombe la Shirikisho FA.
"Tunawafahamu Mbao walitufunga katika mchezo wa nusu FA, hivyo tunafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita na kutojirudia tena... Tunataka kuweka historia ya kuishusha daraja Mbao FC." Alisema Cannavaro
Kwa upande mwingine, timu ya Yanga inatarajiwa kuondoka kesho ijumaa kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo huo wa kufunga msimu wa Ligi kuu