Jumamosi , 5th Mar , 2022

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni amesema waamuzi wanastahili pongezi kwa kuchezesha vema bila kulalamikiwa kwenye michezo ya mwanzo ya mzunguko wapili wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania iliyoanza mzunguko wa 16.

(Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni)

Mwenyekiti Hmaduni amesema “Ni kweli tumemaliza mzunguko wa 16 na kuendelea bila malalamiko, tunashukuru na lazima tupongezane. Ni kwasababu tumejitathmini".

"Katikati ya Ligi waamuzi huwa tuna semina kwa ajili ya kuangalia changamoto zilizojitokeza katika mzunguko wa kwanza ili zirekebishwe na yale maziri tuyashikilie"

"Tunataka kuwafanya waamuzi wetu wawe wanachezesha kwa wingi nje ya nchi, na hatutasita kutoa adhabu pale tunapoona wanakwenda kinyume na inavyotakiwa" alimalizia hivyo Mwenyekiti Nassor Hamduni.

Pongezi hizo zimekuja mapema baada ya waamuzi wa Ligi Kuu kupokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa wadau wa Soka mbalimbali wakiwemo Maafisa wa Serikali juu ya kuboronga kwao kutafsiri sheria 17 za mchezo wa Soka kwenye michezo ya mzunguko wa kwanza.