
Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ya Ballon D’Or
Tuzo za mwaka huu 2025 zitakuwa ni tuzo za 69 zinatolewa na jarida la Ufaransa la France Football ambalo lilianza kutoa tuzo hizi tangu mwaka 1956. Zikiwa ndio tuzo kongwe zaidi katika mchezo wa mpira wa miguu.
Tuzo zitakazo tolewa kwa mwaka huu 2025 zitajumuisha tuzo kubwa ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d'Or kwa wanaume na wanawake, mchezaji bora chipukizi, kipa bora kwa wanaume na wanawake, mfungaji bora ngazi ya klabu/timu ya taifa), Kocha bora wa timu za wanaume na wanawake, klabu bora ya mwaka ya wanawake na wanaume, na tuzo ya mchezaji aliyetoa mchango kwa jamii.
Majina ya wachezaji watakaowania tuzo hizo yatatangazwa mwanzoni mwa Agosti 2025 huku jina la kinda wa Barcelona Lamine Yamal likitajwa zaidi katika kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka upande wa naume.