Wachezaji wa Twiga Stars wakiwa mazoezini.
Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Julai 2 hadi 23, 2022 nchini Morocco ambapo baada ya mchezo wa leo, Twiga Stars watarejeana tena dimbani Oktoba 23, 2021 na mshindi wa jumla atapambana na mshindi kati ya Malawi na Zambia.
Mara ya mwisho kwa mataifa haya kukutana ilikuwa mwaka 2012 katika kutafuta nafasi ya kufuzu Afcon 2012 ambapo Namibia ilipoteza kwa jumla ya magoli 7-2 huku timu zote zikiwa zimewahi fuzu mara moja kwenye Afcon.
Twiga Stars ilifuzu Afcon mwaka 2010 kwa mara ya kwanza ilhali Namibia walipata tiketi ya ushiriki mwaka 2014 kama muandaaji wa mashidano hayo.






