(Timu ya Twiga Stars wakishehereka bao baada ya kuwafunga Sudan Kusini kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B)
Kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Nelson Mandelea Bay nchini Afrika Kusini, Kocha wa timu hiyo Bakari Shime amesema mchezo utakuwa mgumu kwani wawili hao hawajapoteza mchezo hadi sasa.
Kwa upande wa rekodi, Twiga Stars wamecheza na Namibia mara nne, sare tatu zikitawala wakati Namibia akipata ushindi mara moja na kuashiria mchezo huo kuwa utakuwa wenye upinzani mkali.
Mchezo wa nusu fainali ya pili utakaochezwa leo, utawakutanisha wenyeji Afrika Kusini dhidi ya Malawi saa 10:30 jioni na fainali na mchezo wa kumtafuta mshindi watatu imepangwa ichezew Oktoba 9, 2021.






