Ujumbe mzito wa Kapombe kwa wapenda soka

Alhamisi , 8th Aug , 2019

Mlinzi wa klabu ya Simba Shomari Kapombe ametoa shukrani zake kwa mashabiki waliomwombea, baada ya kurejea rasmi uwanjani tangu alipoumia mwishoni mwa mwaka 2018.

Shomari Kapombe

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kapombe ameandika, ''nachukuwa nafasi hii kushukuru kila aliyeshiriki kuniombea''.

Kapombe ambaye alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Power Dynamos ya Zambia Jumanne kwenye Simba Day, ameongeza kuwa, 

''Namshukuru Mungu kwa kila jaribu langu. Nahata pale nilipomkufuru na kulalamika kwa namna yoyote ile hakika ameendelea kuwa mbele yangu'.

Kapombe aliumia kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mwezi Desemba 2018, ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Lesotho.