Ukweli kuhusiana na rasta alizo nazo Mrisho Mpoto

Jumatatu , 25th Nov , 2019

Msanii wa mashairi Mrisho Mpoto maarufu "Mjomba", amesema kitu ambacho hataweza kukifanya ni kuzikata nywele zake aina ya rasta, ambazo anaziona kama ni utamaduni na utambulisho wake kwa watu.

Mrisho Mpoto

Kupitia EATV & EA Radio Digital Mrisho Mpoto amesema hataweza kunyoa rasta zake hadi itakapofikia hatua ya kuwa na uwalaza au labda nywele ziishe kabisa,

"Siwezi kuzinyoa rasta zangu labda watu waje waninyoe usiku, hii ni brand yangu nikijiangalia kwenye kioo naonekana na muonekano mzuri na nazipenda, labda hiki kipara kikiisha na nywele zitakuwa zimeisha ndiyo itakuwa biashara imeishia hapo, lakini zitaisha tu kwa kuwa zimebaki chache" ameeleza.

Mrisho Mpoto ni moja kati ya wasanii ambao wanaheshimika sana katika muziki, na jamii kwa ujumla pia ndiye msanii pekee ambaye utamaduni wake ni kutembea peku popote pale alipo.