Jumatano , 19th Aug , 2020

Golikipa wa zamani wa timu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Uingereza, Joe Hart amejiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs kwa uhamisho huru akitokea katika klabu ya Bunley aliyoitumikia kwa miaka miwili.

Mlinda mlango Joe Hart, akiwa na jezi ya Tottenham Hotpurs baada ya kukamilika kwa usajili wake .

Joe Hart ambaye ameshawahi kuvitumikia vilabu mbali mbali kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester City, Torino ya nchini Italia ,Westham United ya nchini Uingereza kabla ya kujiunga na Bunley  mwaka elfu mbili na kumi na nane.

 

Ametua Tottenham Hotspurs kwa kusaini mkataba wa miaka miwili .

          ATAKACHOKIONGEZA JOE HART TOTTENHAM HOTSPURS
1} KIONGOZI-Ili timu iweze kushinda mataji lazima iwe na kiongozi au viongozi wa kuhakikisha wachezaji wote wanajitoa kwa asilimia mia moja.

Ongezeko la Joe Hart katika klabu ya Tottenham Hotspurs kutaongeza ubora kutokana uwezo wa Joe Hart kuongoza wachezaji wengine akiwemo mlinda mlango namba moja Hugo Lloris ambaye ni nahodha pia mzoefu na mkongwe katika kikosi hicho.

Nyota huyo ameshaitumikia Manchester City na timu ya taifa Uingereza  akiwa nahodha hivyo ataweza kwenda kuongeza kitu katika klabu ya Tottenham kwenye upande wa uongozi wa wachezaji wengine.

2}UBORA .-Joe Hart ni mmoja kati ya magolikipa wazuri sana katika ligi kuu ya nchini Uingereza, ameshawahi kuitumikia timu ya Manchester City kwa ubora mkubwa sana na ameshinda makombe mbali mbali akiwa na timu hiyo kama nahodha.

Kutokana na Golikipa namba mbili wa timu ya Tottenham, Paulo Gazzaniga  kufanya makosa mengi na kushindwa kumpa changamoto Hugo Lloris, Mourinho amemsajili Hart kwenda kuwapa changamoto Lloris na Gazzaniga.

3}UZOEFU.-Joe Hart amecheza mechi nyingi  kwa ngazi ya klabu na ngazi ya Timu ya taifa hivyo kumfanya kua na uzoefu mkubwa , amecheza mechi zaidi ya mia moja  {100}  bila kuruhusu goli na amecheza sabini na tano  {75}  na timu ya taifa ya Uingereza.

Paulo Gazzaniga amekosa kabisa uzoefu ambao ungeisaidia katika mechi kubwa za ligi kuu nchini Uingereza au katika makombe ambayo timu ya Tottenham imekua ikishiriki.

Hugo Lloris amefanya  makosa mengi msimu wa ligi uliomalizika makosa ambayo yameipelekea timu ya Tottenham kupoteza mechi nyingi msimu ulioisha.

USHINDANI .-Joe Hart ataongeza ushindani wa namba katika kikosi cha Tottenham hivyo kutapelekea kupanda kwa viwango wa magolikipa wengine katika klabu hiyo.

Kutokana na kiwango cha Joe Hart kinavyofamika kitamfanya Hugo Lloris kuongeza jitihada mazoezini na kwenye mechi atakazokua anacheza kwani atakua  akijua kuna mtu nje ambaye anaweza kumpokonya namba endapo atafanya makosa kama ya msimu uliopita.