
Sir Jim Ratcliffe - Mmiliki mwenza wa Manchester United
Sir Jim mwenye umri wa miaka 72 utajiri wake umepungua kutoka £23.519bn hadi £17.046bn na kumfanya ashuke kutoka nafasi ya nne hadi ya saba kwenye orodha ya kila mwaka ya watu 350 matajiri zaidi nchini Uingereza.
Kundi la Ineos la Ratcliffe lilinunua hisa za asilimia 27.7 katika klabu ya Manchester United mwezi Februari 2024 kwa mkataba wa thamani ya takriban £1.25bn ($1.6bn) na kupata mamlaka ya kuimiliki klabu hiyo kubwa nchini England
Ikumbukwe wafuasi wengi wa Manchester United wanakosoa uwepo wa bilionea huyo tangu ajiunge na klabu hiyo baada ya United kupandisha bei ya tiketi na kupunguza wafanyakazi katika jitihada za kuboresha kitengo cha fedha katika klabu hiyo