Ijumaa , 8th Dec , 2023

Klabu ya Manchester United inaripotiwa kuwa itawaweka sokoni baadhi ya wachezaji kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2024. Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa watawekwa sokoni ni Casemiro, Raphael Varane na Jadon Sancho.

Kiungo Casemiro kushoto na Rafael Varane kulia huwenda wakauzwa kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2024.

Kwa mujibu wa ripoti kocha wa Manchester United Erik ten Hag atawaondoa baadhi ya wachezaji mwezi ujao kwenye dirisha dogo la usajili barani Ulaya ambalo litafunguliwa tarehe 1 Januari 2024.

Kiungo Casemiro mwenye umri wa miaka 31 na beki Raphael Varane miaka 30 wanatajwa kuwa wataondoka klabu hapo kwa sababu klabu hiyo inakuja na mipango mipya ya sera za usajili hivyo wachezaji hawa wawili hawatakuwa sehemu ya mipango husuani pale mwekezaji mpya Sir Jim Ratcliffe atakapo ingia klabu hapo.

Inaarifiwa kuwa Jadon Sancho ataondoka kutokana na ugomvi wake binafsi na kocha Eric ten Hag na winga huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia.