Jumapili , 31st Jul , 2022

Max Verstappen dereva wa kampuni ya magari ya Red Bull ameshinda mbio za Hangari Grand Prix. Huu ni ushindi wa 8 msimu huu kwa Max kwenye mbio 13 zilizofanyika msimu huu wa 2022 kwenye Langa Langa.

Max Verstappen dereva wa kampuni ya magari ya Red Bull

Kwa ushindi huu wa Leo dereva huyo raia wa Uholanzi amefikisha alama 258 akiwa ndio kinara kwenye msimamo wa madereva na anaongoza kwa tofauti ya alama 80 dhidi ya Charles Leclerc dereva wa Ferrari aliyenafasi ya pili akiwa na alama 178.

Kwenye mbio za leo za Hangarian GP nafasi ya pili na ya tatu wameshika madera kutoka Mercedes Lewis Hamilton nafasi ya pili na nafasi ya tatu imeenda kwa George Russell. Ni mbio za 5 mfululizo Hamilton anamaliza kwenye nafasi 3 za juu msimu huu.