Jumamosi , 16th Oct , 2021

Paula Baldosa atakutana na Victoria Azarenka katika fainali ya michuano ya tenesi ya Indian Wells baada ya nyota huyo kumshinda Ons Jaber siku ya ijumaa.

Victoria Azarenka

Badosa raia wa Hispania ambaye alikuwa akicheza michuano hii kwa mara ya kwanza , alishinda mchezo huo kwa seti mbili za 6-3, 63.

Kwa upande wa Azarenka alitokea nyuma kwa seti moja na kushinda kwa 3-6,6-3,7-5 dhidi ya Jelena Ostapenko.

Azarenka mwenye umri wa miaka 32,anawania kuwa mchezaji wa kwanza mwanamke kushinda taji la michuano hiyo mara tatu baada ya kulitwaa mwaka 2012 na 2016.