Ijumaa , 14th Oct , 2016

Vilabu vya Mpira wa Kikapu nchini vimetakiwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano mbalimbali yajayo ya mchezo huo ili kuweza kuongeza ushindani na kuweza kukuza vipaji kwa wachezaji wapya.

Moja ya mechi katika mashindano ya Kikapu ya Nyerere Cup

Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano ya michunao ya Nyerere Cup Haleluya Kavalambi amesema, mashindano ya mwaka huu yamekuwa na changamoto kubwa ya kiushindani licha ya timu chache kujitokeza hususani kwa upande wa wanawake lakini wanaamini timu zilizojitokeza zimepata fursa ya kujifunza sheria mpya ambazo zitawasaidia katika mashindano yajayo.

Kavalambi amesema, wanaamini mashindano hayo yatazidi kuinua vipaji vipya na vya zamani ambavyo hapo baadaye vitaweza kuonesha ushindani zaidi katika mashindano mbalimbali hapa nchini.