
Akizungumza na EATV Nassoro Hamduni amesema wanafurahishwa na mwenendo bora wa Waamuzi kwenye michezo ya Ligi Kuu huku wakiunga mkono adhabu zinazotolewa kwa Waamuzi ili kuendana na hadhi ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2022-2023.
''Waamuzi wanatakiwa kufata sheria na kanuni za mpira ili kuweza kuondoa malalamiko ya baadhi ya mashabiki na viongozi vilabu ambao wamekuwa hawana imani na maamuzi yao pindi wanapokuwa uwanjani wakichezesha''
Aidha Kamati ya Waamuzi inataraji kuwapiga msasa wa siku 5 waamuzi wote wanaochezesha Ligi kuu Tanzania Bara huku mafunzo hayo yakitaraji kuanza Oktoba 16 mwaka 2022.