Alhamisi , 18th Dec , 2014

Chama cha Riadha nchini Tanzania RT, kimesema ili kuweza kukuza mchezo huo hapa nchini wadhamini wa ndani wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kuukuza mchezo huo na kuweza kuwa na washiriki wengi hususani vijana katika mchezo huo wa riadha.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui amesema wadhamini hao wanatakiwa kutoa sapoti kubwa kwa vijana ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi huku wakiweka imani ya kushinda katika mashindano hayo.

Nyambui amesema mchezo huo hauwezi kukua na kuipa sifa nchi iwapo wadhamini hawataweza kujitokeza kwa ajili ya kuwekeza wakiwa na lengo la kuutangaza.

Nyambui amesema, Tanzania imekuwa ikishiriki mashindano mbalimbali ambayo ni makubwa nje ya nchi, lakini imekuwa vigumu kuweza kufanya vizuri kwenye mashindano hayo kutokana na kukosa wadhamini watakaoweza kuwasaidia kwa ajili ya maandalizi.