Mtibwa Sugar dhidi ya Simba SC
Simba imetinga fainali baada ya kuindoa Azam FC katika mikwaju ya penalti huku Mtibwa Sugar pia ikitinga fainali kwa kuondoa Yanga SC katika mikwaju ya penalti.
Mabingwa wa michuano hiyo tangu mwaka 2007 ni kama ifuatavyo hapa chini.
Mwaka Bingwa Mshindi wa pili Magoli
2007 Yanga SC Mtibwa Sugar (2-1)
2008 Simba SC Mtibwa Sugar (2-1)
2009 Miembeni KMKM
2010 Mtibwa Sugar Ocean View (1-0)
2011 Simba SC Yanga SC (2-1)
2012 Azam FC Simba SC (3-1)
2013 Azam FC Tusker FC (2-1)
2014 KCCA Simba SC (1-0)
2015 Simba SC Mtibwa Sugar (PEN: 4-3)
2016 URA Mtibwa Sugar (3-1)
2017 Azam FC Simba SC (1-0)
2018 Azam FC URA (PEN 4-3)
2019 Azam FC Simba FC (2-1)
Mchezo wa leo wa fainali unatarajia kupigwa kuanzia saa 2:15 Usiku. Je ni nani ataibuka bingwa kati ya Simba inayosaka taji la nne au Mtibwa Sugar inayosaka taji la pili?.