Jumatatu , 25th Oct , 2021

Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher ametoa ushauri kwa bodi ya Manchester United kufanya maamuzi ya haraka ya kutafuta kocha mwingine iwapo kama wanahitaji kutwaa makombe mbalimbali ikiwamo kombe la Ligi Kuu ya Uingereza.

Wachezaji wa zamani wa Klabu za Liverpool na Manchester United, Jammie Carragher(Kulia) na Gary Neville (Kushoto) ambao kwasasa ni wachambuzi wa soka.

Carragher ameyasema hayo baada ya kichapo cha magoli 5-0 kutoka kwa Liverpool walichokitoa kwa United na kusisitiza kwamba kocha wa sasa wa United Ole Gunnar Solskjaer hatoshi kuifundusha klabu hiyo.

“ Ole Gunnar Solskjaer hawezi kushinda ubingwa wa Ligi au Klabu bingwa kama kocha wa Manchester United,hana kiwango sawa na makocha wengine ukilinganisha na makocha kama Jurgen Klopp, Thomas Tuchel or Pep Guardiola” amesema Carragher.

Naye nahodha wa zamani wa United, Gary Neville anaamini kwamba Solskjaer ataendelea kusalia ndani ya United mpaka msimu huu utakapokwisha akipinga maoni ya Jamie Carragher kwamba United haihitaji mwalimu mzoefu kwa muda huu.

“Naamini watasalimia na Ole kwa msimu huu,wanahitaji kushinda makombe wakiwa nae ndani ya msimu huu,usiku huu unaweza kuwa mgumu kwake lakini ukiangalia kilichowakuta makocha kama Mourinho na Luis van Gaal ,hawawezi kumfukuza kocha kwa sasa” alisema Neville.

Huu unakuwa ushindi mkubwa kwa Liverpool kuupata ndani ya Old Trafford tofauti na ule wa October 1895 ambapo Majogoo hao wa Jiji walishinda kwa mabao 7-1 wakiwa Anfield huku hii ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 1955 kwa United kufungwa idadi ya magoli 5 na kushindwa kufunga hata goli moja.

Kichapo cha magoli 5-0 kimeipeleka United mpaka nafasi ya saba kwenye msimamo wa Epl huku kikiwa ni kichapo cha 3 katika michezo 9 ndani ya Epl msimu huu.