Jumapili , 23rd Dec , 2018

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda amekubali ombi la klabu ya Simba la kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Nkana FC kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Haji Manara wa pili kutoka kushoto akiwa na viongozi wa Simba na Nkana FC.

Taarifa ya klabu ya Simba imeeleza kuwa Kakunda ambaye ni mbunge wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora atawaongoza mashabiki wa Simba na watanzania wengine katika mchezo huo ambao ni muhimu kwa Simba.

Katika mchezo huo Simba ambayo ilipoteza 2-1 ugenini inahitaji ushindi wa bao 1-0 au zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya mkaundi ya michuano hiyo.

Joseph Kakunda

Simba ikishinda mchezo huo itakuwa imerudia historia yake ya mwaka 2003 katika michuano hiyo ambapo iliwatoa mabingwa watetezi Zamalek ya Misri na kutinga hatua ya makundi.

Simba sasa ndio timu iliyobaki kwenye michuano ya kimataifa baada ya wawakilishi wengine ambao ni Mtibwa Sugar kutolewa jana kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 5-1 na KCCA ya Uganda.