
Nape amesema, anamatumaini Yanga na Azam watafanya vizuri kwani wanajua jinsi wanavyozidi kusonga mbele ndivyo wanavyokutana na timu nzuri zaidi kuliko zile walizocheza nazo na kufanikiwa kusonga mbele.
Nape amesema, watanzania wanatakiwa kuwapa moyo katika kuiwakilisha nchi ili timu hizo ziweze kufanya vizuri zaidi katika muendelezo wa michuano hiyo.
Yanga itakutana na Al Alhy ya Misri baada ya kufanikiwa kusonga mbele katika raundi michuano hiyo ya Klabu bingwa Afrika baada ya kuitoa APR kwa kuichapa bao 3-2 ambapo katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa Uwanja wa Amahoro nchini Rwanda Yanga iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 huku katika mchezo wa marudiano Yanga ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya APR Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa Azam FC inayoshiriki kombe la Shirikisho kombe la Shirikisho Afrika itakutana na Esperance ya nchini Tunisia katika mchezo wa raundi ya pili kati ya Aprili 8-10 mjini Dar es salaam na kurudiana Aprili 19 au 20 mjini Tunis.