Jumanne , 7th Sep , 2021

John Terry na Michael Owen ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya England walionza mazungumzo na Mkuu wa maendeleo ya mpira wa FIFA, Arsene Wenger juu ya mabadiliko makubwa kwenye kalenda ya mechi za kimataifa.

Arsene Wenger

Kocha huyo wa zamani wa Arsenal anaongoza kikao hicho kinachohusisha mada ya kufanyika kombe la dunia kila baada ya miaka miwili badala ya minne kama ilivyokua tangu uzinduzi wake mwaka 1930.

Mnamo mei, Wenger alisema kuwa angetamani kuona Mashindano ya mataifa ulaya pamoja na kombe la Dunia yakifanyika kila baada ya miaka miwili, huku Rais wa FIFA Gianni Infantino akiunga mkono wazo hilo ingawa wanakumbana na vikwazo vikali kutoka kwa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Kwenye kikao hicho kimehudhuriwa na magwiji wengi wa soka kama Ronaldo De Lima na Sami Khedira ambao washawahi kushinda Kombe la dunia kwa nyakati tofauti.