
Michuano ya wazi ya Australia ambayo imeanza kushika kasi yake hii leo.
Licha ya kutatizwa na maumivu ya goti siku za hivi karibuni Serena mwenye umri wa miaka 34 ambaye ndiye kinara kwa ubora kwa wanadada duniani amepata ushindi wa seti za 6-4 7-5 dhidi ya muitaliano Camila Giorgi kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Kwa upande wa Djokovic ambaye ndiye kinara kwa ubora duniani ameshinda mbele ya mkorea Hyen Chyng kwa seti za moja kwa moja za 6-3 6-2 6-4.
Nyota wengine kama Roger Federer kwa wanaume na Maria Sharapova kwa wanadada watashuka dimbani hii leo kwenye mechi zao za kwanza za ufunguzi.