Jumanne , 21st Apr , 2026

Klabu ya Wolverhampton Wanderers, maarufu kama Wolves, imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi Kuu England (EPL) na kurejea Championship baada ya matokeo ya suluhu kati ya West Ham United na Crystal Palace hapo jana usiku kuthibitisha hatima yao.

Wolves wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 17 pekee baada ya mechi 33. Tofauti ya pointi 16 kutoka eneo salama (safe side) huku zikiwa zimesalia mechi tano pekee ambazo hata wakishinda hawawezi kujiokoa kutoka nafasi ya kushuka daraja.

Katika msimu huu, Wolves walikumbwa na mwanzo mbaya baada ya kushindwa kushinda mechi zao 19 za kwanza, hali iliyowafanya kubaki kwenye hatari ya kushuka kwa muda mrefu. Licha ya kupata ushindi muhimu baadaye, juhudi hizo hazikutosha kubadili mwelekeo wa msimu wa mashindano wa 2025/26.

Kushuka kwao daraja  kunahitimisha safari ya miaka nane ya Wolves ndani ya EPL tangu walipopanda daraja mwaka 2018. Sasa klabu hiyo italazimika kujipanga upya kwa ajili ya ushindani wa Championship msimu ujao.