(Msemaji wa Yanga, Haji Manara na Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli)
Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema klabu hiyo hairidhishwi na mwenendo wa kimaamuzi kwa baadhi ya waamuzi huku vilabu vingine vikinyimwa haki zao za matokeo na hawaoni hatua yoyote zikichukuliwa na mamlaka husika kuhusu vitendo hivyo.
"Kuna matukio yasiyopungua tisa (9) mpaka 10 yanayohusisha mechi za Simba ambayo yanalalamikiwa na watu kama wanavyolalamika kwa mechi zingine, hatuna shida na neno la kusadikika la waamuzi nao ni binadamu lakini jambo hilo basi liwe kwa timu zote sio kwa klabu moja pekee" amesema Manara.
Naye mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya Yanga Hassani Bumbuli amesema mlolongo wa matukio wa kimaamuzi yenye utata yanayoendelea kutokea kwenye ligi ya NBC premier league hayaleti afya njema kwenye ligi yetu ambayo ni ya 10 kwa ubora barani Afrika huku lengo lao ni kuwataka na kuwakumbusha waamuzi kujitafakali upya .



