Yanga yaanza kupangua ratiba ya Ligi

Jumatatu , 9th Sep , 2019

Bodi ya ligi nchini (TPLB), imebadilisha ratiba ya mchezo Namba 17 wa ligi kuu kati ya wenyeji Mbeya City dhidi ya Yanga.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtendaji mkuu wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, imeeleza kuwa sababu ni kuipa nafasi Yanga kujiandaa na mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco ya Zambia.

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa inaonesha kuwa mchezo WA Yanga na Zesco utapigwa Septemba 14, 2019 jijini Dar es salaam.

Yanga tayari imeshacheza mechi moja ya ligi kuu na kufungwa 1-0 na Ruvu Shooting.