Jumapili , 24th Jan , 2016

Yanga SC imefuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kuichapa mabao 3-0 Friends Rangers jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga SC imefuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya kuichapa mabao 3-0 Friends Rangers jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva aliifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kona ya Issoufou Boubacar.

Msuva tena akafunga bao la pili dakika ya 23 kwa ufundi baada ya kupokea pasi safi ya mshambuliaji Paul Nonga ambaye naye alipenyezewa pasi muruwa ya Salum Telela.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga walipata bao la tatu dk ya 51 likifungwa na mshambuliaji Matheo Anthony kwa kichwa, akimalizia krosi ya Salum Telela.

Kwa ushindi huo, Yanga SC inaungana na mahasimu, Simba SC ambao walifuzu jana kwa kuichapa Burkina Faso mabao 3-0 mjini Morogoro.

Matokeo mengine ya kombe hilo la TFF iliyopigwa hii leo ni pale Njombe Mji ilipoenda suluhu dhidi ya Prisons (Prisons ameshinda kwa penalti 5-3, Amaan, Njombe),wakati Stand Untd akilala 0-1 dhidi ya Mwadui FC (Kambarage, Shinyanga).

Kesho michuano hiyo itaendelea kwa Kagera Sugar dhidi ya Rhino Rangers (Mwinyi, Tabora),huku Panone FC dhidi ya Madini (Ushirika, Moshi) wakati African Lyon ikishuka na Azam FC (Karume, Dar es Salaam).