Jumanne , 28th Jan , 2020

Klabu ya Yanga imetangaza kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama wake utakaofanyika Jumapili, Februari 16, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Makao makuu ya klabu ya Yanga

Mkutano huo utakuwa na ajenda takribani sita ikiwemo ajenda kubwa ya kuwasilisha, kuainisha na kupigia kura marekebisho ya katiba ya klabu hiyo.

Katika taarifa rasmi ya klabu hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mshindo Msolla, ajenda zitakazojadiliwa ni kama ifuatavyo:

- Kufungua mkutano
- Kuthibitisha akidi ya mkutano
- Kupitisha ajenda ya mkutano
- Kuainisha na kuwasilisha mapendekezo ya (Katiba iliyo sasa/mapendekezo mapya)
- Kupigia kura mapendekezo ya marekebisho ya katiba
- Kufunga na mwisho wa mkutano