Jumapili , 25th Oct , 2020

Klabu ya soka ya Yanga, imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa jioni ya leo Oktoba 25, 2020 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la pili.

Licha ya kutanguliwa na KMC kwa goli la dakika ya 27 lililofungwa na Hassan Kabunda, lakini Yanga walisawazisha na kuongeza goli la ushindi hivyo kujinyakulia pointi tatu.

Goli la kusawazisha la Yanga lilifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 41, kupitia mkwaju wa penati. Goli la pili likafungwa dakika ya 61 na mshambuliaji Waziri Jr.

Mchezaji Waziri Jr wa Yanga akimtoka mchezaji wa KMC FC

Yanga sasa imefikisha pointi 19, kwenye mechi 7 ikiwa nafasi ya pili, nyuma ya Azam FC ambayo inaongoza ligi kwa alama 21 kwenye mechi 7.

Mshambuliaji Waziri Jr, sasa amecheza mechi 60 za ligi kuu soka Tanzania bara na amefuna magoli 34.