Alhamisi , 14th Jan , 2021

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela amethibitisha kuwa tayari klabu hiyo imeshafanya malipo kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yao dhidi ya mchezaji Bernard Morrison kwenye mahakama ya usuluhishi wa michezo Duniani CAS.

Klabu ya Yanga inaamini Bernard Morrison ni mchezaji wao halali

Kauli hiyo ameiota muda mchache baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi hapo jana ambapoMakamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela aliiambia EATV kuwa wameshafanya malipo kwa ajili ya kesi hiyo.

 

“Jana ilikuwa ni deadline ya malipo, sisi kama klabu ya Yanga tulisema tumedhamilia kupata haki na malipo tulishafanya kwa hiyo tunasubiria kupangiwa kesi itafabyika lini” amesema Mwakalebela

 

Klabu ya Yanga ilikata rufaa kwenye mahakama ya usuluhishi wa michezo Duniani CAS juu ya kutoridhishwa na maamuzi ambayo yalitolewa na kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la mpira a miguu nchini TFF, juu ya uhalali wa mkataba wa mchezaji Bernard Morrison na klabu ya Yanga.

 

Ikumbukwe kesi hiyo ilimfanya Morrison kuishinda Yanga na kuachwa kuwa mchezaji huru na baadae akajiunga na klabu ya Sim ba SC.

 

Hapo juzi, Januari 12 ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kufanya malipo kwa ajili ya kesi hiyo kupangiwa jaji na siku ya kusikilizwa kwenye mahakama hiyo, ambaye iliweka wazi kuwa mchezaji Bernard Morrison anakesi yakujibu.