Yanga yamalizana na CAF

Ijumaa , 10th Aug , 2018

Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Omary Kaaya, ameanika hadharani orodha ya wachezaji ambao usajili wao ulikuwa haujakamilika katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Wachezaji wa klabu ya Yanga wakiwa mazoezini.

Kaaya amewataja wachezaji hao kuwa ni Matheo Athony, Mkongomani Herieter Makambo pamoja na Deus Kaseke ambaye alisajiliwa kutokea Singida United.

Yanga imefanikisha kukamilisha usaili wa wachezaji hao ambapo Makambo ameongezeka baada ya kukosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Gor Mahia uliofanyika Jumapili ya Agosti 29 jijini Dar es Salaam.

Wakati Makambo akiongezeka kwenye orodha ya wachezaji ambao usaili wao CAF umekamilika, kikosi kipo mjini Morogoro hivi sasa kiiendelea na mazoezi. Yanga imepiga kambi ya wiki mbili kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa Agosti 19 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.