Yanga yatoa ripoti ya wachezaji wake

Alhamisi , 21st Nov , 2019

Klabu ya soka ya Yanga, imetoa ripoti juu ya wachezaji ambao ni majeruhi na waliorejea dimbani baada ya kupona.
Kupitia taarifa yake leo, Yanga imesema wachezaji watatu kati ya watano waliokuwa majeruhi, wamerejea kikosini na wako tayari kwa majukumu.

Wachezaji wa Yanga

Wachezaji hao ni Lamine Moro, Mohammed Issa 'Banka' na Ally Ally. Huku wachezaji ambao bado wanaendelea na matibabu ni Paul Godfrey 'Boxer' na Juma Mahadhi.

Katika kujiandaa na mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara kesho dhidi ya JKT Tanzaania kocha wa Yanga Boniface Mkwasa amesema timu ipo vizuri.

"Baada ya mazoezi ya leo, vijana wangu wako tayari kwa ajili ya mchezo. JKT Tanzania ni moja kati ya timu nzuri naamini utakuwa mchezo mzuri  sana, vijana wapo tayari kimwili na kiakili kuwakabili wapinzani wetu na kuondoka na pointi tatu hapo kesho." - Charles Boniphace Mkwasa.