
Mwinyi Zahera (kushoto) na Haruna Moshi
Katika kikosi cha kwanza cha Yanga kitakachocheza dhidi ya Mbeya City jina la Haruna Moshi lipo, hivyo atacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu akiwa na Yanga.
Usajili wa Boban ndani ya Yanga ulikuwa ni pendekezo la moja kwa moja la kocha Mwinyi Zahera ambaye mara nyingi amekuwa akimsifia kuwa ni miongoni mwa viungo bora kwenye ligi kuu msimu huu.
Boban amesajiliwa katika dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka huu akitokea klabu ya African Lyon ambayo inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi.
Kabla ya mchezo wa leo unaopigwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa TPL ikiwa imecheza mechi 17 bila kufungwa ikijikusanyia alama 47.
Kikosi kamili cha leo.
1. Ramadhani Kabwili
2. Paul Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Abdallah Shaibu
5. Kelvin Yondani
6. Feisal Salum
7. Ibrahim Ajibu
8. Haruna Moshi
9. Heritier Makambo
10. Amissi Tambwe
11. Mrisho Ngassa