Jumatatu , 9th Mei , 2022

Vyama shirikishi vya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kikiwepo chama cha Walimu, Chama cha Umoja wa Mabondia, Waamuzi, Wakuzaji na Mawakala wa ngumi za kulipwa nchini wametakiwa kujipanga na kuhakikisha wanafanyia kazi na kuziondoa changamoto zilizojitokeza na zilizopo katika

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’, Sajenti Seleman Kidunda

Rai hiyo imetolewa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi na Afisa michezo mwenye dawati la vyama hivyo vya ngumi za kulipwa wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Allen Alex, wakati wa uchaguzi wa vyama hivyo shirikishi vya kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini.

"Katiba zenu hazijitoshelezi, nendeni mkakae mziangalie kwa jichonla pili, mkishindwa njooni baraza msaidiwe kuna wataalam,"amesema Allen Alex.

Aliendelea kwa kuwataka kukaa na kuamua aina ya wanachama wao ndani ya vyama vyao kwa kuzingatia makundi yote bila kunyima haki za makundi mengine pamoja na kuwawakilisha vyema wanachama wao kwa kamisheni.

Aidha, amewataka chama cha wakuzaji na mawakala kuhakikisha wanalipa ada za mwaka kabla ya kufika tarehe 14 Mei siku ya uchaguzi wa TPBRC wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kutokulipa ada za serikali watakosa uhalali wa kupiga kura katika kamisheni hiyo.

Kwa upande wao viongozi waliopatikana katika uchaguzi huo wameishukuru BMT kwa kuratibu uchaguzi huo na kuahidi kushirikiana na wanachama wao kwa mujibu wa katiba na kanuni zao pamoja na sheria Baraza kwa maendeleo ya mchezo huo nchini.