Jumatano , 5th Oct , 2022

Kikosi cha wachezaji 25 wa Azam FC kinataraji kuondoka kesho Alhamisi ya Oktoba 6,2022 kuelekea jijini Benghazi,nchini majira ya Saa 11.25 Alfajiri kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022-2023..

Azam FC

Miongoni mwa nyota 25 wanaosafiri kuelekea Libya ni pamoja na Ali Ahmada,Lusajo Mwaikenda,Bruce Kangwa, James Akaminko,Sospeter Bayana,Aggrey Morris,Iddi Nado na Yahya Zayd.

Azam FC wataikabili klabu ya Al Akhdar ya Libya mnamo Oktoba 08-2022 siku ya Jumamosi majira ya Saa 2:00 Usiku huku nyota 7 wakiwemo  Wilbol Maseke,Kenneth Muguna,Ibrahim Ajib ,Ismail Aziz Kader,Shaaban Idd Chilunda na Rodgers Kola wakiachwa kwenye safari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zinazowakabili.