Jumatano , 24th Jan , 2024

Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC ambaye ni Raia wa DR Congo Mwinyi Zahera amesema Taifa Stars haiwezi kuifunga Congo katika mchezo wa leo kuwania kufuzu kuingia 16 bora katika fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2023 yanayoendelea nchini Ivory Coast.

Leo Stars inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya DR Congo iliyotoka kugawana pointi mojamoja na timu ya taifa ya Morocco ambayo iliifunga Tanzania mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Ikiwa Stars itapata ushindi leo itafikisha pointi nne, kama Zambia itapoteza dhidi ya Morroco angalau kutakuwa na nafasi ya kutinga 16 bora ikishinda matumaini yatayeyuka.

Ipo wazi kuwa pointi moja waliyopata Tanzania ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Zambia walifunga bao la mapema dakika ya 11 kupitia kwa Simon Msuva katika dakika za lala salama Zambia iliweka usawa na kufanya ubao kusoma 1-1.