Afisa Elimu wa shule za msingi Halmashauri ya mji wa kahama Aluko Aluko.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na kuvifungia vituo hivyo, afisa elimu shule za msingi katika halmashauri hiyo, Aluko Lukole, amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na kubaini uwepo wa vituo vinavyotoa mafunzo kwa mfumo wa shule za awali kinyume na taratibu za uendeshaji wa shughuli hiyo zikiwamo taasisi za dini.
Lukole amevitaja vituo hivyo ni Mpondi academy, Nyakato parent nursery and day care, Royal daycare na kituo cha EAGT cha kanisa la EAGT mtaa wa Mbulu kata ya
Mhongolo.
Vituo vingine ni Chery center, Lighting future, Debla pre and primary school, Umahat Islamia, Tumaini pre and primary school, Sister Cecilia and Amedeus, Mwangaza center, Wazazi nusery school, New Salama english and nursery school na Shunu academy.
Aidha, amesema vituo hivyo vyote havina hadhi ya shule kutokana na kuendeshwa kwa mfumo ambao siyo halali na anayetaka kuanzisha shule ni lazima afuate taratibu kwa kupitia mamlaka husika ambayo ni ofisi ya mkurugenzi na ofisi ya mdhibiti wa ubora wa elimu.
Lukole ameongeza licha ya kutotambulika na mamlaka husika, vituo hivyo vingine vinaendeshwa na watu ambao si raia wa Tanzania, vituo kuendeshwa katika mazingira hatarishi kwa watoto, ukosefu wa usalama wa kutosha kwa watoto pamoja na uendeshaji wa mafunzo kinyume na mfumo wa mitaala ya elimu hapa nchini ikiwa ni kinyume na taratibu wa uendeshaji wa elimu nchini.
Hata hivyo, amewataka wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla kwenda katika ofisi za elimu halmashauri hiyo ili kupata maelekezo ya sehemu sahihi ya kuwapeleka watoto wao na siyo kufuata mkumbo wa mikusanyiko ya watoto ambayo haina utambuzi sahihi na mamlaka inayosimamia masuala ya elimu.