Jumatatu , 28th Mar , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema mabalozi wa nyumba kumi watumike kuimarisha ulinzi na usalama katika mitaa yao ikiwemo kuwabaini wageni wanaowatilia shaka.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga

Mkuu wa mkoa huyo amesema hayo ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Geita, na kusema matukio ya uhalifu yanawakwaza wananchi na serikali imeamua kuimarisha amani na utulivu katika mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita meja generali mstaafu ezekiel kyunga ameagiza ushiriki wa wananchi katika masuala ya ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya wilaya mpaka mtaa kuimarisha uhusiano na mabalozi wa nyumba kumi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita meja generali mstaafu ezekiel kyunga amewataka wanaomiliki silaha taasisi za ulinzi na wadau wengine mkoani humo wapeleke silaha katika vituo vya polisi vilivyopo karibu kwenda kuhakikiwa kabla ya mwisho wa mwezi wa juni .