Jumatano , 20th Jul , 2016

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Rebeca Gyumi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amesema vijana wengi nchini hawaamini katika kujitolea kwanza ili kufikia malengo na mafanikio.

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Rebeca Gyumi

Bi. Rebeca ambaye alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga sheria ya ndoa ya mwaka 1976 ambayo inatoa mwanya kwa watoto wa kike kuolewa kabla ya umri wa miaka 18, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha SUPAMIX kinachorushwa na East Afrca Radio.

‘’Vijana wengi hawapendi kujitolea vitu kwa ajili ya jamii yao ndiyo maana tulipofungua kesi hiyo vijana wenzetu walituiambia kwamba nyie mtakuwa mmepewa hela siyo bure’’ Amesema Rebeca.

‘’Sisi tuliomba tusilipe gharama za kesi kwa kuwa suala hilo ni la kijamii na Mahakama Kuu ilipitia shauri hilo na kuona umuhimu wa suala hilo kwa kuwa watoto wanaoolewa mapema ni wa wananchi hasa maskini’’ Amesema Rebeca

Hata hivyo Rebeca amesema kuwa ndoa za utotoni kwa wasichana ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri mdogo ni chanzo kikubwa cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.

Kwa upande wake wakili ambaye alisimamia kesi hiyo Jebra Kambole amesema Ibara ya 26 ya Katiba inaruhusu mwananchi kuweza kueleza kwamba ameona sheria mfulani inakiuka misingi ya jamii na kuomba marekebisho jambo ambalo walitumia nafasi hiyo kuweza kuandaa shauri hilo.