Kocha huyo amesema japokuwa ligi imekuwa ngumu lakini wanamatumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC waliowatangulia nafasi moja mbele katika msimamo wa ligi.
"Tunacheza na Azam FC katika uwanja wao...Wachezaji wangu wote kiafya wapo vizuri, tangu tumeanza Ligi tumekuwa washindani mpaka hii leo tupo nafasi ya nne tukiwa tumepishana pointi mbili na wapinzani wetu Azam FC ambao wapo nafasi ya tatu na tunataka tushindane ili tuipate nafasi ya tatu. Hata mwakani tujipange upya tuwe katika ushindani wa kuwania Ubingwa". Alisema Jangalu
Pamoja na hayo kocha huyo amewataka waamuzi wa michezo kuchezesha mechi hizo za mwisho kwa kufuata sheria zote za Soka ili kuhakikisha mshindi anapatikana kihalali katika kila mchezo.