Jumapili , 20th Aug , 2017

Balaa la bomoa bomoa lililowakumba wakazi wa Kimara Suka jijini Dar es salaam linaendelea kuchukua sura mpya, baada ya wizara zinazohusika kuanza kutupiana mpira.

Tukio hilo ambalo ambalo limetekelezwa na wakala wa ujenzi wa barabara nchini TANROADS, limeacha wananchi wengi wakazi wa eneo hilo wakiwa kwenye majonzi na vilio, huku familia zao zikibaki hazina makazi.

East Afrika Radio ilipotafuta viongozi wenye dhamana na masuala ya makazi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ilifanikiwa kumpata Naibu Waziri wa wizara hiyo Mh. Angelina Mabula, na kusema kuwa wao kama wizara hawajaletewa malalamiko au taarifa rasmi, hivyo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ndio wahusika rasmi la suala hilo.

"Masuala ya barabara yana mipaka yake katika mipango yao waliyonayo, na ungeweza kupata jibu zuri zaidi kama ungeweza kuwaona watu wa wizara ya ujenzi, kwa sababu bado lipo kwenye mikono yao, na hakijatufikia kwetu sisi", alisikika Angelina Mabula akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio.

East Africa Radio ilipowatafuta watu wenye dhamana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano haikufanikiwa kuwapata kwa mara moja, huku simu ya Waziri huiska Mh. Makame Mbarwa ikiita bila kujibiwa.

Msikilize Naibu Waziri Mabula hapa chini..

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mh. Angelina Mabula