Jumapili , 20th Aug , 2017

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mh. John Wegesa Heche, anatafutwa na jeshi la polisi mkoani humo, kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi mpaka sasa.

Mbunge wa Tarime Vijijini John Wegesa Heche.

Akithibitisha taarifa hizo msemaji wa CHADEMA Bw. Tumaini Makene, amesema John Heche alimetakiwa kufika polisi leo hii jioni, muda ambao anatarajia kuwa na mkutano wa hadhara.

"Hizo taarifa zina ukweli na mpaka sasa hivi hao polisi hawataki kusema wanamuhitaji wa nini, tena wanamuhitaji muda ambao anatarajia kuwa na mkutano wa hadhara, yani kama wana lengo la kuzuia huo mkutano usifanyike, kwa sababu hawasemi ni nini", alisema Tumaini Makene akizungumza na mwandishi wetu wa habari.

Wakati huo huo Tumaini Makene ametoa taarifa juu ya afya ya mbunge wa Bunda Mjini Ester Amos Bulaya, kuwa hali yake si nzuri akiwa huko mahabusu kwani presha yake imeshuka, na kwamba hajaoka tangu alivyopelekwa jana.

Jana Ester Bulaya alikamatwa na polisi kwa kosa la kuhudhuria mkutano wa mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, na mpaka sasa hajaachiliwa, huku mwenzake John Heche akitafutwa na polisi.